YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA PILI CHA WIZARA YA ELIMU NA WAWAKILISHI WA MADARASA NA IDARA
Kikao Kilifanyika Tarehe 12/04/2019 Katika chumba cha
Darasa namba 9. Kikao kilihudhuriwa na Wawakilishi wa Madarasa yaani (CR’s) na
Wawakilishi wa Idara mbalimbali yaani (DR’s);
Pia Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MISO) Mh. Aziz Juma Hamad na Waziri Mkuu Mh. Athuman Bakene Walialikwa na kufika katika Kikao hicho.
AJENDA
Ø
Kufungua Kikao
Ø
Utambulisho
Ø
Kusoma Muhtasali wa kikao kilicho
pita
Ø
Yatokanayo na kikao kilicho pita
Ø
Uwajibikaji
Ø
Kufunga kikao
Baada ya kikao kufunguliwa na Waziri wa Elimu Mh. Kanal Seif Waziri Mkuu alipewa
nafasi ya kuongea machache ambapo alionge kuhusu (01) Viongozi kuwa wazalendo
na Serikali yao (02)Uhamasishaji wa watu kufanya mazoezi (03) Nafasi ya
kiongozi.
Baada ya hapo Waziri Mkuu Alimkaribisha Rais nae
azungumze machache na Rais Alizungumza yafuatayo; 01: Kiongozi kuwa mfano na kioo kwa jamii 02:
Kujenga utamaduni wa kujifunza 03: Kujengana ndani ya Ungozi 04: Ahadi zilizo
tekelezwa na Serikali ya Wanafunzi (MISO).
CHANGAMOTO
Ø
Wajumbe Kutoka Majimbo tofauti
walitoa changamoto zifuatazo nakuonekana ni kikwazo katika suala zima la
Taaluma kwa wanafunzi wao;
Ø
Stationery ya MISO kutofunguliwa
mapema
Ø
Kusumbua kwa SRMIS na watu kushindwa
kuona Course work zao
Ø
Baadhi ya Walimu kuwasumbua watoto wa
kike kwa matakwa yao binafsi
Ø
Changamoto ya viti katika Cr4,5,6,7,8
na Cr9
Ø
Baadhi ya Wanafunzi kutopata
vitambulisho vyao
Ø
Ukosefu wa taa LT5
Ø
Kuchelewa kwa fedha ya mawasiliano
MWISHO
Waziri wa Elimu Mh. Kanali Seif aliwashukuru wajumbe
kuhudhuria katika kikao hicho na kuwa ahidi kuzitafutia ufumbuzi changamoto
zote zilizo tajwa na wajumbe, na kuahidi kufanya vikao vingine vya wizara ya
Elimu ili kuleta mrejesho wa changamoto zilizo tolewa na wajumbe.
Kikao Kili ahirishwa rasmi saa, 02:08 Usiku
Written By Eston T. Msigala







No comments: